Business Technology & Consulting 

Mkoa wa Pwani ndio mkoa ulio tengwa rasmi kwa ajili ya viwanda nchini Tanzania, ni mkoa wa viwanda. Takwimu zinaonesha kuwa mkoa huu kufikia mwaka 2018 una idadi ya viwanda vipatavyo 1500(elfu moja na mia tano) vikiwemo vipya vilivyo anzishwa hivi karibuni ambavyo idadi yake yapata 450.

Kauli Mbiu: Viwanda Vyetu Uchumi Wetu.

Wiki ya viwanda mkoani Pwani iliambatana na ziara ya Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu, alipata kutembelea viwanda mkoani huko ikiwa ni mwendelezo wa kuitaka/kuwataka watanzania kuwekeza na kutunza viwanda vyetu vya ndani ili kupatia Taifa pato na kukuza uchumi wetu.

Kilele cha Maadhimisho haya yalifanyika katika viwanja vya sabasaba na kuhudhuriwa na Waziri wa biashara na viwanda hon. Charles Mwijage, wakuu wa wilaya, wawezeshaji na wadhamini pamoja na viwanda mbali mbali vidogo kwa vikubwa, vipya na secta za serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viwanda na washiriki walipatiwa maeneo/mabanda kwa kuonesha bidhaa na kuweza kutangaza bidhaa zao kama fursa ya pamoja ili kuwezesha kujulikana kwa viwanda hivi.

Hizi zote zikiwa ni juhudi za Rais wetu wa awamu ya tano, Mtukufu Dr. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati na kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025. Hakika Tanzania ya viwanda Inawezekana.

Katika hotuba ya Makamu wa Rais aliye mwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye maadhimisho haya aliwataka watanzania kujiamini na kulinda viwanda vyetu kwa tukimuunga mkono Rais katika kufanikisha kusudi hili jema kwa manufaa ya nchi/uchumi wetu na vizazi vijavyo. Pia, alisisitiza kuna bidhaa tunaagiza nje aghalabu sisi wenyewe twaweza kuzalisha katika viwanda vya hapa hapa ndani na kupeleka nje pia kuzingatia ubora na umaridadi katika uzalishaji jambo ambalo lingeongeza pato la Taifa..

Singo Africa Limited ilipata fursa ya kuhudhuria maadhimisho haya kwa siku tatu mfululizo kujifunza na kumuunga mkono Rais wetu katika Kuhakikisha Tanzania ya viwanda inawezekana.

Singo Africa Limited pia ilipata kutembelea viwanda mbali mbali katika kutaka kuwafahamisha juu ya matumizi ya mifumo ya tehama kwa ajili ya uendeshaji wa viwanda vyao katika kuwasaidaia kutunza kukumbuku za uzalishaji, mapato/uhasibu, manunuzi, mauzo na mahusiano na wateja wao. Katika kusaidia hili

Singo Africa Ltd hutoa huduma ya mfumo wa TEHAMA mahususi kabisa kwa ajili ya viwanda na imejikita rasmi kuhakikisha viwanda vyetu vina rekodi(kumbukumbu) nzuri katika kuvisaidia kufanya maamuzi mazuri kwenye nyanja zote zikiwemo za ukuaji, maendeleo na kustahimili katika soko.

Tanzania ya viwanda inawezekana kabisa huku tukiamini viwanda vyetu uchumi wetu bila kusahau matumizi mazuri ya TEHAMA (Software) madhubuti kwa ajili ya viwanda.

Kwa wamiliki wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, kipya au endelevu Singo africa Ltd ipo tayari kukusaidia katika kuhakisha unakuza biashara yako na kupanua soko katika zama hizi za Teknologia.

0
0
0
s2sdefault